TIMU YA TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA FEASSSA 2024 – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Watu Wazima, Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Elimu Maalum, na Michezo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ernest Hinju, leo Agosti 16, 2024, amekabidhi bendera ya Taifa kwa timu za wanafunzi, walimu, na viongozi wanaoenda kushiriki katika Mashindano ya 22 ya Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA). Sherehe hiyo imefanyika katika Chuo cha Ualimu Tarime, Mkoani Mara.

Hinju aliwataka washiriki wote kujituma na kutumia umahiri wao katika kila mchezo, huku wakitambua kuwa wanabeba dhamana ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo muhimu. Aliwasihi kudumisha upendo, umoja, na mshikamano, akisisitiza kuwa michezo hiyo itakutanisha nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya, na Uganda.

Mashindano ya FEASSSA 2024 yanatarajiwa kuanza kesho, tarehe 17 hadi 27 Agosti 2024, katika mji wa Mbale, Uganda. Tanzania itawakilishwa katika michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, hockey, tennis, riadha, mpira wa mikono, na netiboli. Timu ya Tanzania imejizatiti kufanya vizuri na kuleta ushindi kwa Taifa.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts