ZNZ yazipa sekta binafsi kuendesha spitali zote ,dawa na matibabu bure ZNZ

Kwa miaka mingi huduma za Afya za Zanzibar zikiendelea kua bure kwa vipimo vyote huduma kubwa na ndogo ,Waziri wa afya wa Zanzibar Nassor Mazrui ametangaza Hospitali zote Zanzibar zilizojengwa na Rais mwinyi sasa rasmini zitasimamiwa na sekta binafsi kwenye uwendeshaji ili kua na huduma za kimataifa

Mazrui amesema Wizara ya Afya imeingia makubaliano maalum ya Uwendeshaji na usimamizi na sekta binafsi Ikiwemo EHN na TCL na kusisitiza kua Wizara ya Afya haikubinafsisha Bali ni kuongeza ufanisi wa Hospitali hizo ikiwemo za Wilaya na za Mikoa ili wananchi kupata huduma Bora

“Tumebaini kua wananchi wengi wanapenda kwenda spitali binafsi na wanapoteza fedha nyingi ,wengine hawana wanaopenda kwa wafadhili wasaidiwe ,kuwaondolea shida hiyo wananchi sisi tunawalipa sekta binafsi kwa niaba yao ili wapate huduma matibabu bila ya malipo ,watu wanatibiwa na kupata dawa zote na vipimo bila ya malipo yeyote na serikali inawalipa sekta binafsi wanaotoa huduma katika spitali–Mazrui”

Related Posts