Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Namungo dhidi ya Fountan Gate umesogezwa mbele kutokana na utata wa usajili uliotokana na kifungo Cha Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).
Mchezo huo ulikuwa upigwe leo saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Majaliwa kabla ya Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) kuiandikia barua Namungo juu ya uamuzi huo.
Namungo ilikuwa tayari imejiandaa na mchezo huo kabla ya jana jioni kupokea taarifa ya TPLB juu ya kuahirishwa kwa mchezo huo.
“Tulikuwa tumeshajiandaa na mchezo, lakini jana tukapokea hiyo taarifa kwamba mchezo hautaweza kuchezwa kutokana hayo mambo ya Fountgate,” amesema mmoja wa mabosi wa juu wa Namungo.
Tatizo kubwa lililouondoa mchezo huo ni kutoka na Fountan Gate kushindwa kufanya usajili wowote katika dirisha lililopita kutokana na kufungiwa na FIFA.
Timu hiyo ina kesi za madai na waliokuwa wachezaj waliovunjiwa mikataba bila kufuata utaratibu ambapo hadi dirisha la usajili lilipofungwa Agosti 15, timu hiyo haikuwa imesajili wachezaji wapya huku ikiwa na wachezaji watano pekee waliokuwa msimu uliopita.
Inaelezwa kuwa Fountain Gate imekwamishwa na staa wao mmoja wa zamani ambaye licha ya kumlipa fedha, lakini FIFA imeshindwa kuthibitisha malipo hayo kufanyika kutoka kwa wanasheria.