MKUU WA MAJESHI; “WAPE SALAMU ZANGU WAMENIFURAHISHA SANA KWA MATOKEO MAZURI”

Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda, ameipongeza shule ya sekondari Ruhuwiko inayomilikiwa na jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania JWTZ, kupata matokeo mazuri mitihani ya kidato cha Sita mwaka 2024.

Hayo yamesemwa na mkuu wa 401 kundi la vikosi Meja Jenerali Charles Peter Feruzi wakati wa sherehe iliyoandaliwa na shule ya sekondari Ruhuwiko kwaajili yakumpongeza kupanda cheo kutoka Brigedia Jenerali hadi Meja Jenerali, ambapo amesema Mkuu wa Majeshi ametoa salamu kwa shule hiyo kwani imemfurahisha kwa matokeo waliyoyapata ya kidato cha Sita.

Amesema kuwa wanafunzi hao wanatakiwa kujikita zaidi katika kuongeza ufaulu kwa vita pekee wanayotakiwa kuishinda ni Ile yakitaaluma, kwakuhakikisha wanapata matokeo mazuri hususani wanafunzi walio katika madarasa ya mitihani.

Mkuu wa kikosi cha Jeshi 411 KJ, Ruhuwiko Christopher Andrew Rugeimukamu amesema kufuatia aliekuwa Brigedia Jenerali Charles Peter Feruz kupanda Cheo nakuwa Meja Jenerali, hiyo inadhihirisha kuwa amekidhi vigezo na ndio maana ameaminiwa na Mh. Rais pamoja na mkuu wa majeshi kupata nafasi hiyo.

Katika sherehe hiyo ambayo imefanyika shuleni hapo yenye lengo la kutoa pongezi na shukuran zao za dhati kwa kipindi chote ambacho wamekuwa wakifanya nae kazi kama mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo na ahadi Yao kubwa ikiwa nikuendelea kufaulisha wanafunzi wengi zaidi kama ambavyo ilikuwa ni maono ya kiongozi huyo.

Akizungumza Mkuu wa shule ya sekondari Ruhuwiko Luteni Kanali Benedictor Bahame amesema kuwa Meja Jenerali amekuwa msaada mkubwa Sana kwenye shule hiyo, na kwa umoja wao wamefanikiwa kuisaidia shule kufikia ufaulu mkubwa ukilinganisha na ufaulu wa awali kabla hajaanza kuiongoza shule hiyo.

Aidha amesema walifanikiwa kuwa shule ya Tisa Tanzania kwa kuongeza ufaulu wa hali ya juu jambo ambalo likichagiza zaidi maendeleo ya shule hiyo ambayo mpaka hivi sasa imekuwa ikifanya vizuri nakufanikiwa kufaulisha wanafunzi wengi kwa madaraja ya juu.

Amesema shule hiyo haifanyi mzaha na wanataka kuifanya iwe shule iliyobora ambayo inatoa elimu kwa gharama nafuu zaidi “Ruhuwiko sekondari Mafuriko ya division 1” amesema Luteni Kanali Benedictor Bahame.

Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Meja Jenerali kupata nafasi hiyo, pamoja na ushirikiano ambao ameuonyesha walipokuwa wakifanyakaz pamoja kama mwenyekiti wa bodi hiyo ambapo amemtaka kuendelea kuikumbuka shule hiyo huku akiahidi kuendelea kuyaenzi mazuri yake kwa kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kufanya vizuri zaidi kitaaluma kama ilivyokuwa maono yake.

Akizungumza kwa niaba ya bodi ya shule Yusuph Mwikoki amesema wazazi wametimiza wajibu wa kuwapeleka wanafunzi shuleni pamoja na walimu wametimiza wajibu wakuwafundisha vizuri hivyo wanafunzi hao wanajukumu lakuleta matokeo mazuri kwa shule kwa kuwa naufaulu mzuri.

Ameeleza kuwa awali akiwa Brigedia Jenerali Alikuwa na msimamo wakusimamia na kuhakikisha wanafunzi wanakuwa naufaulu mzuri hivyo ktk kuyaenzi mema aliyoyafanya enzi akiwa mwenyekiti wa bodi hiyo Meja Jenerali Charles Peter Feruzi ni kuona wanafunzi wanaendelea kupata matokeo mazuri.


Related Posts