Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Makunduchi
KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam imekabidhi jezi 100 kwa mashabiki wa Simba walioko Kizimkazi katika Wilaya ya Kusini visiwani Zanzibar.
Jezi hizo zimekabidhiwa leo Agosti 17,2024 kwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mwenyekiti wa Mwanamke Initiatives Foundation Wanu Hafidh Ameir ambaye atakabidhi jezi hizo kwa wananchi ambao ni mashabiki wa Simba.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Kwa jezi hizo , Mbunge Wanu Hafidh Ameir amesema walichokifanya Simba ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na amewapongeza kwa uamuzi huo.
“Tunapongeza Simba Kwa kutoa jezi hizi ambazo tunakwenda kuwabidhi mashabiki wa hapa kwetu.Ni jambo nzuri na linapaswa kuwa la mfano.Niwaombe na vilabu vingine kuiga mfano huu wa Simba wawe wanarudisha kwa Jamii,”amesema Wanu.
Amesisitiza katika kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi limekuwa na matukio mengi yanayoendelea Kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo katika jamii lakini leo kutakuwa na tukio la mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga.
Kuhusu mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga,Wanu amesema mwaka 2023 hakupatikana mshindi hivyo mechi ya leo itakuwa na mvuto wa aina yake.
Hata hivyo amesema huu ni mwaka wa pili wa Tamasha la Kizimkazi na huko mbeleni wataangalia namna ya kuboresha Kwa kuongeza timu nyingine ambazo nazo zinapendwa na zinamashabiki wengi.
Awali kabla kukabidhi jezi hizo , Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba CPA Issa Masoud amesema kuwa wanatambua kuwa Simba iko katika jamii na hivyo inayonafasi ya kurudisha kwa jamii na leo imekabidhi jezi hizo 100 kama sehemu ya kutambua jamii hasa ya wapenda michezo.
“Tunawaojibu wa kufanya Kwa ajili ya jamii inayotutazama ,hivyo Kwa niaba ya Klabu ya Simba leo tunakabidhi jezi 100 kama sehemu ya kurudisha kwa jamii ambayo imekuwa ikitushabikia.”
Mwenyekiti wa Mwananke initiatives Foundation Wanu Hafidh Ameir ambaye pia ni Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akipokea jezi za Simba kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba CPA .Issa Masoud .Jezi hizo zimekabidhiwa leo Makunduchi katika Wilaya ya Kusini ambako pia kunafanyika mchezo wa mechi ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga