Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha ZFF, Awadh Maulid Mwita ameahidi kutoa donge nono kwa timu za Uhamiaji na JKU ambazo ni wawakilishi wa Zanzibar katika mechi za kimataifa.
Awadh amesema timu hizo mbili iwapo zitapata ushindi katika mchezo wa kwanza basi kila moja itapewa Sh 1 Milioni na zikitapata sare basi ataipatia Sh 700,000.
Ameongezea pia, timu ambayo itapata ushindi kwenye mchezo wa pili (marudiano), basi ataizawadia kitita cha Sh1 Milioni.
JKU inaiwakilisha Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika itacheza na Pyramids ya Misri kesho Agosti 18, saa 2:00 usiku kwenye Uwanja wa 30 June Air Defence Stadium.
Wakati huo Uhamiaji FC wawakilishi wa Zanzibar wa Kombe la Shirikisho itashuka uwanjani kuvana na Al Ahli Tripoli ya Libya saa 2:00 usiku kwa Saa Afrika kwenye Uwanja wa Tripoli International Stadium.