VIKAO VYA CHAMA RUDISHENI WAGOMBEA WANAOUZIKA KWA WANANCHI

NA WILLIUM PAUL, SAME.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (MCC) Fadhili Maganya amevitaka vikao vya Chama ngazi ya kata, wilaya na mkoa kukirahisishia chama hicho kwa kuwaleta wagombea wanaouzika kwa Wananchi.

Maganya alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Ndungu wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo alisema kuwa, lengo la chama ni kuheshimu maamuzi ya Wananchi.

Alisema kuwa, kitendo cha vikao vya chama ngazi zote kupitisha majina ya wagombea ambao wanauzika kwa wnanachi itapelekea chama kushinda kea kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

Aidha Mwenyekiti huyo amewataka Watumishi wa umma kukisaidia chama cha Mapinduzi kukitafutia kura za kishindo kwa kutatua kero za wananchi kwa kuwafuata vijijini na sio kukaa ofisini pekee.

Alisema kuwa, wilaya ya Same ni miongoni mwa wilaya ambayo haina migogoro baina ya chama na serikali na kuwataka kuendelea kushikamana na kushirikiana katika kuwatumikia Wananchi.








Related Posts