11 WAKAMATWA KWA MAKOSA YA UTAPELI NA KUPATIKANA NA MENO YA TEMBO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kufanya utapeli kwenye nyumba ya watawa wa kike, eneo la Bigwa Sisters Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoani humo,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Alex Mkama amesema Agosti 16, 2024 watuhumiwa hao waliingia ndani ya eneo hilo na kunadi madini bandia kwa ajili ya kujipatia kipato, pia walijitambulisha kuwa ni watafiti wa mali kale na kwamba eneo hilo ni sehemu ya utafiti wao.

Katika tukio lingine mkoani humo watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na vipande 29 vya meno ya tembo katika Wilaya ya Kilosa.

Related Posts