ASILIMIA 53 YA TAASISI ZA UMMA TANZANIA ZATUMIA MFUMO WA e-OFFICE KUTUNZA KUMBUKUMBU – MWANAHARAKATI MZALENDO

Asilimia 53 ya taasisi za umma nchini Tanzania sasa zinatumia mfumo wa ofisi mtandao (e-office) katika utunzaji wa kumbukumbu na usimamizi wa nyaraka za kidijiti, hatua ambayo imeongeza ufanisi katika utendaji kazi wa serikali.*

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, Xavier Daud, wakati akifungua Mkutano wa 59 wa Bodi ya Baraza la Wahifadhi Nyaraka Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESARBICA), uliofanyika jijini Arusha mnamo Agosti 19, 2024.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutumia mfumo wa kidigitali kwa kutumia e-office, ambao unarahisisha wananchi kupata huduma kwa haraka, hasa katika taasisi za umma. Mfumo huu unasaidia sana katika usimamizi wa kumbukumbu za kidijiti na pia unachangia kukusanya maoni na malalamiko ya wananchi kwa njia ya kidijiti kupitia e-mrejesho,” alisema Daud.

Rais wa ESARBICA, Puleng Kekana, aliwasihi wanachama wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo kwa wataalamu wa kumbukumbu, hasa vijana, ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora na utunzaji mzuri wa kumbukumbu kwa faida ya jamii.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts