Hakuna Madini ya Tanzanite yatatoka mirerani bila kupitia Tanzanite exchange centre -Waziri Mavunde

Waziri wa madini Antony Mavunde amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa zikidai kuwa jengo linalojengwa la billion tano halitatumika tena kufanya biashara ya madini ya Tanzanite pamoja na kuongeza thamani ya madini hayo huku akisema Rais ameongeza fedha ambazo zinaingia leo na litajengwa hadi kufikia asilimia 99

Mavunde akizungumza na wafanyabiashara wa madini,wachimbaji na wadau wengine wa sekta hiyo ndani ya geti amesema hakuna Madini ya Tanzanite yatatoka mirerani bila kupitia Tanzanite exchange centre

Mbunge wa simanjiro mkoani Manyara amemshangaa mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kuhoji maelekezo ya Rais kuhusu madini ya Tanzanite kuendelea kuuzwa mirerani

Sendeka akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya ukuta wa mirerani ukihusisha wafanyabiasha pamoja na waziri wa madini amesema biashara hiyo haipaswi kufanyika Arusha kwenye vijiwe kama ilivyopendekezwa na wadau mbalimbali bali biashara na uongezaji wa thamani vinatakiwa vifanyike ndani ya ukuta na baada ya kuongezwa thamani yauzwe kwenye masoko ya nje.

Related Posts