Dar es Salaam. Kesi ya ukahaba inayomkabili, Amina Ramadhani na wenzake 17 imeshindwa kuendelea na ushahidi baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Sokoine Drive, Francis Mhina kuhamishwa katika mahakama hivyo.
Washtakiwa hao wanadaiwa wakati wanakamatwa walikuwa wamevaa mavazi yasiyo ya heshima, ambayo ambayo ni kiashiria cha vitendo vya ukahaba.
Akizungumza mbele ya Hakimu Mfawidhi, Rachel Kasebele, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Regina Kayuni amedai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, lakini hakimu anayeendesha shauri hilo amehamishwa.
“Tunaiomba Mahakama iharishe shauri hili hadi tarehe nyingine kwa kuwa hakimu anayeendesha kesi hii amehamishiwa,” amesema Kayumi.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mfawidhi Kasebele amekubaliana na maombi ya upande wa Jamuhuri na kuahirisha hadi Agosti 27, 2024.
“Maombi ya upande wa Jamuhuri nimeyasikia, kutokana Hakimu anayeendesha shauri hilo amehamishiwa hivyo naahirisha hadi Agosti 27, 2024.
Hadi sasa waliotoa ushahidi katika kesi hiyo ni mashahidi wawili akiwemo Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Kipolisi Magomeni na Edward Mwasunga.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Aisha Iddi, Mariana Sia, Mwajuma Hamza, Mariamu Hassan, Najma Hamisi, Sabrina Gabriel, Mariam Kitamoga, Elizabeth Michael.
Wengine ni Rosemary John, Recho Kindole, Lobi Daudi, Diana David, Jackline Daniel, Mwajuma Bakari, Jenifa John, Zainabu Hamisi na Recho Bakari.
Washtakiwa hao wanadaiwa wakati wanakamatwa walikuwa wamevaa mavazi ya si ya heshima ambayo ni kushiria cha vitendo vya umalaya.
Katika kesi hiyo, inadaiwa Juni 14, 2024 katika maeneo ya Sinza Mori Wilaya ya Ubungo Dar es salaam washtakiwa wote walikutwa na tuhuma ya wakijiweka katika namna ambayo sio sawa mbele za umma na kufanya vitendo visivyofaa na kuvaa mavazi yasiyokubalika kwa nia ya kufanya ukahaba.