LIGI Kuu England imeshuhudia wafungaji mahiri sana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Baadhi ya mastaa walionasa Kiatu cha Dhahabu kwa maana ya kuongoza kwa mabao kwenye ligi ni pamoja na Mohamed Salah, Harry Kane na Erling Haaland huku viungo kama Bruno Fernandes na Kevin De Bruyne wakiongoza kwenye kupika mabao hayo.
Kwa miaka mitano iliyopita, kuna mastaa wameonyesha kwamba wao ni hatari kwa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu England, huku Haaland akiingia kwenye orodha hiyo licha ya kutua kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka 2022.
Kwa takwimu za mabao kwa miaka mitano iliyopita kwenye Ligi Kuu England, hii hapa ndiyo orodha ya wakali 20 waliofunika kwenye jambo hilo la kutumbukiza mipira nyavuni.
1. Mohamed Salah (Liverpool, mabao 101)
2. Harry Kane (Tottenham, mabao 86)
3. Son Heung-min (Tottenham, mabao 78)
4. Erling Haaland (Man City, mabao 64)
5. Ollie Watkins (Aston Villa, mabao 59)
6. Jamie Vardy (Leicester City, mabao 56)
7. Callum Wilson (Bournemouth
9. Marcus Rashford (Man United,
10. Raheem Sterling (Chelsea, mabao 54)
11. Phil Foden (Man City, mabao 53)
12. Danny Ings (Southampton, Aston Villa & West Ham, mabao 50)
13. Diogo Jota (Wolves & Liverpool, mabao 49)
14. Chris Wood (Burnley, Newcastle & Nottm Forest, mabao 49)
15. Bukayo Saka (Arsenal, mabao 48)
16. Gabriel Jesus (Man City & Arsenal, mabao 45)
17. Kevin De Bruyne (Man City, mabao 45)
18. Sadio Mane (Liverpool, mabao 45)
19. Jarrod Bowen (West Ham, mabao 43)
20. Dominic Calvert-Lewin (Everton, mabao 43)