Dar es Salaam. Meli zinazopeperusha bendera za China na Ufilipino zimegongana leo Jumatatu, Agosti 19, 2024 karibu na mwamba unaogombaniwa katika Bahari ya Kusini ya China.
Kulingana na vyombo vya habari vya Serikali ya Beijing, China inaishutumu Manila kwa kusababisha ajali hiyo kwa makusudi.
Msemaji wa walinzi wa Pwani ya China, Gan Yu amesema:“Meli ya walinzi wa Pwani ya China ilijaribu kuzuia meli ya Ufilipino kufika Sabina Shoal.”
Meli ya Ufilipino inadaiwa kwenda njia isiyo ya kitaalamu na ya hatari, hivyo kusababisha mgongano.
Katika shutuma zake hizo, Yu amesisitiza hatua ya meli hizo kugongana ilikuwa ya makusudi na kwamba Ufilipino ndio inayohusika zaidi.
Wakati China ikitoa shutuma hizo, Mamlaka nchini Ufilipino imezipinga vikali ikisema mgongano huo umetokana na kile alichokiita:”Ujanja usio halali na wa fujo” wa walinzi wa Pwani wa Uchina.
Ikumbukwe, hilo ni tukio la kwanza katika miongo kadhaa kwa nchi hizo mbili kupigana juu ya Sabina Shoal.
Sabina Shoal ni miamba iliyozama nusu maili 86 kutoka kisiwa cha Ufilipino cha Palawan, zaidi ya maili 30 karibu na Palawan kuliko Second Thomas Shoal, ambapo meli ya Ufilipino ilizuiliwa.
Kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya habari