PSPTB YAFUNGA MAFUNZO YA TAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Amani Ngonyani amefunga Semina ya ‘Research Workshop’ iliyokuwa na lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yaliyoanza  Agosti 12 hadi Agosti 16, 2024.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka PSPTB Amani Ngonyani aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi amesema wanafunzi wa Bodi wanapaswa kuwa waaminifu kwenye sehemu za kazi ili serikali iweze kupata kodi stahiki ili kufikia malengo yaliyowekwa hasa kuhudumia wananchi.

Ngonyani amesema Bodi hiyo iko macho na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wanaokiuka maadali ya Taaluma ya Ununuzi na Ugavi kwakuwa hivi karibuni imeonekana kuna udanganyifu mkubwa kwenye manunuzi hivyo hawatasita kuwachukulia hatua.

Aidha amewasisitiza watu ambao ni wazoefu kazini kuwaelekeza waajiliwa wapya kwenye maeneo ya kazi taratibu na njia mbaya zinazokiuka mienendo na maadili ya taaluma ya Ununuzi na Ugavi.

Pia amesema hii itaweza kusaidia kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuondoa lawama ambazo zinaweza kutolewa kwa Serikali ikiwemo kulaumiwa na matendo ambayo yanatendwa na watendaji ambao wameaminiwa kuweza kufanya kazi kwa niaba ya hao wananchi.

Leo baada ya kuhitimu mafunzo ya siku tano wahitimu wamepewa vyeti vya kuonesha ushiriki wao katika mafunzo hayo ili kuanza kuandika research proposal/ mapendekezo ya tafiti zenu mapema iwezekanavyo.

Wanafunzi wa Bodi zaidi ya 100 wameshiriki mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) yaliyoanza Agosti 12 hadi Agosti 16, 2024 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza na wenyeji Dar es Salaam.

Related Posts