Wanne wanaodaiwa kuwa majangili wakamtwa na Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro na vipande 29 vya meno ya Tembo

Watu wanne wanaodaiwa kuwa majangili wamekamtwa na Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na vipande 29 vya meno ya Tembo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika operation maalum ya kupambana na vitendo vya kihalifu wa malialisili katika hifadhi zilizopo mkoani Morogoro

Kamanda mkama amesema serikali inafanya jitihada kubwa katika kukuza Sekta ya utalii nchini hivyo baadhi ya watu wamekua walirudisha nyuma hivyo Jeshi Hilo kushirikiana na Jeshi la uhifadhi wataendelea kulinda Malisili zilizopo Ili zilete mafanikio.

RPC Mkama amewataka watuhumiwa walikamatwa ni Yahaya Bakari (60) Mkulima mkazi wa chalinze Mashina Mlugu Ntumbi (41) Mkulima mkazi wa Mlenge vianzi Juma Ramadhan Zinga (46) Mkulima mkazi wa Bagamoyo Mansour Juma Abdallah (40) Mkulima mkazi wa Dar es salaam

Hata hivyo jeshi la polisi limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya kihalifu na kuacha tamaa ya Mali kwa Njia zisizo halali

Related Posts