Ni Agosti 20, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika kutoa vyeti ya mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Uwanja wa Mwehe Makunduchi Visiwani Zanzibar.
Katika Tukio hilo Rais aliwakabidhi vyeti wahitimu wa mafunzo ya Kilimo Biashara, Ujasiriamali pamoja na Utalii.
Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya unywaji na uuzaji wa Maziwa nchini Ahmed Asas alipata nafasi ya kuzungumza namna fursa na unufaikaji watakaoupata Wana Kizimkazi kupitia kampuni yake ya Asas.
‘Mheshimiwa Rais kuambatana na Elimu hii sio tu walipata Elimu Darasani lakini kama Asas tuliweza kuleta Ng’ombe wa Maziwa wa kisasa pamoja na Mbuzi wa nyama wa kisasa na kondoo ili Wanafunzi waweze kufanya Theory na Practical’- Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Asas, Ahmed Asas
‘Mheshimiwa Rais zana ya Mafunzo hayo ya Mifugo kuwawezesha Wafugaji wa Kizimkazi na viunga vyake waweze kufuga kisasa na kufuga kibiashara, kama tunavyoelewa Zanzibar ina fursa kubwa sana na soko kubwa sana la nyama na maziwa’- Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Asas, Ahmed Asas
‘Lakini bila kuwapatia Wafugaji hawa Elimu ya ufugaji wa kisasa na Ufugaji wa mbegu bora ya ng’ombe itakuwa ni vigumu sana kupata masoko ya bidhaa bora ya mifugo’- Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Asas, Ahmed Asas
‘Kuona muamko ni mkubwa sana Mheshimiwa Rais hivyo tumeshauriana na Kamati ya maandalizi ya Elimu haya ya Kizimkazi Wanafunzi hawa leo hii waliopata Elimu ya mifugo tutawalika mashambani kwetu Iringa watagharamikiwa na Kampuni ili sasa waweze kujifunza mnyororo mzima kuanzia upandaji wa mifugo jinsi ng’ombe wanavyokamulikwa hadi mazima yanavyochakatwa kiwandani’-Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Asas, Ahmed Asas
‘Mwisho na kipekee Mheshimiwa Rais nikushukuru wewe binafsi na Serikali yako kwa kuwezesha mazingira bora ya Ufugaji tumekuwa tunaona Tasnia ya mifugo kila mwaka tunaweza kushindana na nchi jirani na wafugaji wa kubwa, kati na wadogo wamehamasika kufuga kisasa nikushukuru na kazi iendelee’-Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Asas, Ahmed Asas