DC KASILDA AYANYOOSHEA KIDOLE MASHIRIKA BINAFSI.

NA WILLIUM PAUL, SAME.

MKUU wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewataka wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwenye utendaji kazi wao hasa pale inapotokea wanapata ufadhili kutanguliza uzalendo kwa nchi kwanza.

Alisema kuwa, kumeshuhudiwa mara kadhaa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia NGOs kueneza mambo ambayo yapo kinyume na taratibu za nchi ikiwemo kuharibu maadili ya vijana.

Kasilda amezungumza hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambapo kwenye Wilaya hiyo kuna jumla ya NGOs 39 ambazo zinashirikiana na Serikali kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Awali Kaimu Mkurigenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Charles Anatol amesema NGOs yeyote itakayobainika kufanya shughuli zake kinyume na katiba zao inavyomtaka zipo sheria ambazo zitachukuliwa na Serikali ya Wilaya ikiwemo kusitisha utekelezaji wa shughuli za Shirika ndani ya Wilaya.

Kwaupande wake Adam Henry ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali Wilaya ya Same (NaCoNGO) amesema kufanyika kwa mkutano huo kila mwaka kunatoa fursa kwa wamiliki wa NGOs kujadili namna shughuli za mashirika zinavyoweza kwenda sambamba na mipango ya kitaifa.




Related Posts