Planet yaichapa CUHAS | Mwanaspoti

Timu ya kikapu ya Planeti imeichapa CUHAS kwa pointi 74 -52 katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA) kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Mirogo.

Michezo mingine iliyochezwa uwanjani hapo ilizikutanisha Profile iliyoifunga Young Profile kwa pointi 74-59 na Eagles ikaifumua Cross Over kwa pointi 68-44.

Akizungumzia michezo hiyo, kocha maarufu wa kikapu mkoani Mwanza, Benson Nyasebwa aliwapongeza wachezaji  chipukizi wanaoshiriki ligi hiyo kutokana na namna wanavyocheza.

Nyasebwa ambaye pia ni katibu msaidizi wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF), alisema kuwepo kwa chipukizi wengi kutawafanya wapate wachezaji bora watakaowakilisha timu ya taifa siku zijazo.

Related Posts