MINAPA kuwashirikisha wananchi mapambano ya Ujangili na utunzaji hifadhi yatimiza miaka 60

Katika kuelekea kilele Cha maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi wafanyabiashara wa soko la Green lilipo katika mji huo wamempongea uongozi wa hifadhi hiyo kwa kushiriana katika shughuli za kijamii ambapo wamefanya usafi ndani ya soko Hilo ambalo lilionekana kusahaulika kwa kipindi Cha muda mrefu huku wakiiomba Serikali kuwaboreshea soko hilo kwani hadi sasa Miundombinu hairidhishi

Wakizungumza Baada ya kufanya usafi katika eneo Hilo wafanyabiashara wamesema kuwa soko hilo ndo soko pekee ambalo linawapatia kipato huku baadhi ya watu wengi kutokuriridhishwa na ilivyo hali ambayo inasababisha wateja wengi kukimbia eneo hilo

Kwa Upande wake Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Mikumi kamishina msaidizi wa uhifadhi Augustine Massesa amesema kuwa zoezi hili kitakuwa endelevu ili kuhakikisha wanaboresha mazingira yanayozunguka hifadhi hiyo sambamba na kuwashirikisha wananchi masuala Mbalimbali ya hifadhi ikiwemo kupambana na ujangili,uchomaji moto hivyo.

Pia amesema kuwa kuongezeka kwa idadi ya watalii kumekuwa ni chachu ya wao kushirikikiana na jamii ili kuhakikisha namba ya watalii inaongezeka zaidi

Kwa Upande wake kamishina msaidizi mwandamizi wa uhifadhi John Nyamhanga Mkuu wa Kanda ya masharki amesema wataendelea kushukiriana na wananchi na kama hifadhi itahikisha inaboresha mazingira yote ambayo yamesahaulika

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilianzishwa tangu mwaka 1964 na Kilele Cha maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi kinatarajia kufanyika mnamo agosti 31 huku ikihudhuriwa na wadau na Viongozi ikiambatana na michezo mbalimbali

Related Posts