RAIS WA ZANZIBAR AZUNGUMZA NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA NCHINI TANZANIA MHE. CHRISTINE GRAU IKULU ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Mhe.Christine Grau,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 21-8-2024.

(Picha na Ikulu)

Zanzibar,

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuweka mkazo zaidi kwenye sekta ya mwani ili kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuzipatia soko la uhakika.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Ulaya nchini, Tanzania, Christine Grau.

Alisema, asilimia 99 ya wakulima wa zao la mwani Zanzibar ni wanawake, hivyo alimueleza balozi huyo kuangalia haja ya kuwaungamkono wanawake na wakulima wa mwani nchini hasa kwa mafunzo na vifaa kisasa ili wazalishe mwani wenye ubora utakaoendana sambamba soko la uhakika.

Mbali na mambo mengine ya maendeleo na uwekezaji ikiwemo utalii, Rais Dk. Mwinyi pia alimueleza Balozi Grau kuwa Uchumi wa Buluu ni sera kuu ya Uchumi wa Zanzibar hivyo alimueleza kuangalia fursa zinazotokana na sera hiyo.

Pia Rais Dk. Mwinyi ameupongeza Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano mzuri uliopo na Tanzania na kueleza kuwa wameshirikiana kwa miaka mingu kupitia sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo, Elimu, maji, afya na miundmbinu.

Kwa upande wake Balozi Christine Grau amesifu juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi na kueleza kuwa wanafanyakazi kwenye maeneo mbalimbali iliwemo kushirikiana jamii kupitia serikali za mitaa na taasisi za kiraia (NGO’s) kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii Unguja na Pemba.

Ameeleza kupitia mradi wao wa “Green City” wamesaidia masuala ya Jinsia hasa kuwawezesha wanawake kwenye Elimu, Uchumi ikiwemo Uvuvi, pamoja na masuala ya uongozi wa fedha.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

Related Posts