VIJIWE vya Bodaboda vya jijini Dar es Salaam na Dodoma vinatarajiwa kuchuana katika soka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani nchini.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Ramadhan Ng’azi ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 21, 2024.
Kamanda huyo alikuwa akizungumzia maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa barabarani yanaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Usalama Barabarani.
Kamanda Ng’azi amesema michezo hiyo itaanza Agosti 26-30, mwaka huu katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma na kauli mbiu ni endesha salama fika salama.
Amesema bodaboda ni sekta inayokuwa kwa kasi na pia inaaminika na Watanzania lakini wenyewe hawajaona huko kuaminika.
“Kabla kutatanguliwa na mechi kabambe ya miguu, hivi karibuni mkoa wa Dodoma uliendesha mashindano kuanzia ngazi ya kijiwe hadi ngazi ya wilaya wakapata mshindi,” amesema.
Amesema mashindano hayo yalifanyika katika ngazi ya mkoa wakapata mshindi ambayo ni Wilaya ya Kongwa.
“Wilaya ya Kongwa walishinda na wakawa ni bodaboda wanaochabanga mpira waguu. Shirikikisho la jiji la Dar es Salaam watakuja hapa kwa treni ya SGR na watakabidhiwa zawadi kubwa sana,” amesema.
Amesema watatumia wasanii katika kuburudisha na kuelemisha wananchi kuhusu matumizi bora ya barabara wakiwemo singeli na mashairi ya kufoka foka, huku akimtaja mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.