AFANDE ANAYETAJWA KWENYE TUKIO LA BINTI WA DOVYA ACHUKULIWE HATUA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI), umeungana na Watanzania, watetezi wa haki za binadamu hususani haki za wanawake na wasichana katika kukemea ukatili wa kijinsia aliofanyiwa binti mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam.

 

 

 

Mtandao huo umetoa maazimio yake yaliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Transforming Life, Nashivai Mollel ambapo wametaka uwajibikaji wa Jeshi la Polisi, kwa kumchukulia hatua ‘afande’ anayetajwa kuhusika katika kuwatuma vijana watano kutekeleza ukatili huo.

 

 

 

Pia wameshauri mawakili watakaowatetea watuhumiwa kuepuka kumuumiza zaidi binti huyo kwa kusimamia misingi ya haki na utu wa binti.

 

 

 

Wametaka uchunguzi zaidi wa makosa kwani yaliyotajwa ni machache wakati kuna ushahidi wa video unaoonesha makosa mengi zaidi, ikiwemo ubakaji wa kundi, usafirishaji wa mtoto kingono, ulawiti, kula njama za kutekeleza uhalifu, kuteka nyara na shambulio la kudhuru.

 

 

 

 

Pia wamelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mtuhumiwa mwingine ambaye anadaiwa kuwa chanzo cha ukatili huo kwa kuwa na mahusiano na binti huyo, mwanaume ambaye anadaiwa kuwa hawara wa afande ili awajibike kwa kufunguliwa mashitaka ya usafirishaji wa kingono chini ya kifungu cha 6 (1) 6 (4) cha sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu sheria namba 6\/2008 ikisomwa pamoja na sheria ya nyongeza namba 2\/2022.

Related Posts