JKT Stars yaifunga DB Lioness

TIMU ya mpira wa kikapu ya JKT Stars iliishinda timu ya DB Lioness   kwa pointi 64-52 katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika kwenye Uwanja wa Donbosco Oysterbay.

Timu ya JKT Stars ikiongozwa na Jesca Ngisaise,  ilianza mchezo huo kwa kasi hali iliyofanya iongoze  katika robo ya kwanza kwa pointi 24-11.

Robo ya pili ilivyoanza DB Lioness ilibadilika na  kupata pointi 16-9 na hadi kufikia mapumziko washindi walikuwa mbele kwa pointi 33-27.

Robo ya tatu JKT Stars  ilipata pointi 14-11, 17-11.

Katika mchezo huo, Jesca Ngisaise aliongoza kwa kufunga pointi 34, kati ya pointi hizo alifunga pointi 21 kwa mitupo saba ya pointi tatu-tatu (three pointers).

Aliyemfuatia alikuwa Penina Mayunga aliyefunga pointi 8, na kwa upande wa DB Lioness alikuwa Taundencia Katumbi aliyefunga pointi 17.

 Michezo mingine iliyochezwa uwanjani hapo timu ya Tausi Royals iliifunga Mgulani Stars kwa pointi 64-44 na kwa upande wa wanaume UDSM Outsiders iliifunga   Chui kwa pointi 62-41.

Related Posts