Makambo atamba kuwajaza tena | Mwanaspoti

BAADA ya kurejea tena nchini kwa mara ya tatu, mshambuliaji wa Tabora United, Heritier Makambo, ametamba mapema kwamba awamu hii amekuja kivingine na kutaka kurejesha heshima mbele ya mashabiki wanaokikubali kipaji alichonacho hasa kwa ile staili ya kuwajaza kila alipotupia mpira nyavuni.

Makambo amejiunga na Tabora akitokea Al Murooj ya Libya, japo hakuanza mechi dhidi ya Simba, lakini anatamani kufanya vitu vikubwa msimu huu, ili kurejea katika kiwango alichonacho.

Mchezaji huto alitua nchini mara ya kwanza akijiunga na Yanga Julai 1, 2018 akitokea FC Lupopo ya DR Congo, akaondoka Agosti 10, 2019 akiwa amefunga mabao 17 Ligi Kuu kisha kujiunga na Horoya ya Guinea. “Kwanza nitaanza kupambania tuzo za mchezaji bora wa mwezi, ambazo naona ni fursa kwa wachezaji kuamsha ari ya kujituma na wakijua kuna watu wanathamini wanachokifanya.

“Kurejea kwa mara nyingine Tanzania, natamani kurejesha heshima na thamani yangu ambayo niliiweka msimu wangu wa kwanza, naamini itawezekana kwa kujituma na nipo tayari kujitoa kwa ajili ya timu yangu.” 

“Najua nimerejea timu ambayo ni tofauti na Yanga, ili mladi nikipata nafasi ya kucheza, nitafanya mambo makubwa,” alisema aliyerejea tena msimu misimi iliyopita kuichezea Yanga lakini hakuwika kabla ya kutumkia Libya.

Related Posts