MCHEZAJI Amin Mkosa wa timu ya Mchenga Stars anaongoza katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kwa kuiba mpira kutoka kwa wapinzani wake (steal) akifanya hivyo mara 40.
Kuiba mpira (steal) kama inavyoitwa, inatokana na mchezaji kunyakua mpira kutoka kwa mpinzani wake bila ya kumfanyia madhambi.
Mchezaji anayemfuatia katika kipengele hicho ni Evance Davies kutoka UDSM Outsiders aliyeiba mara 37, Sixto Ngomeni (Mgulani JKT) mara 36, Tyrone Edward (UDSM Outsiders) mara 30, Starley Mtunguja (Ukonga Kings) mara 27 na Alinani Msongele (ABC) 27.
Mkosa anayecheza namba 3 Power forward anaongoza pia kwa kufunga pointi 410, akifuatiwa na Jonas Mushi kutoka JKT aliyefunga 393.
Wachezaji wengine ni Tyrone Edward (Outsiders) 385, Stanley Mtunguja (Ukonga Kings) 357, Alfan Mustafa (Vijana) 342 na Jamery Marbuary (Dar City) 340.
Wengine ni Fotius Ngaiza (Vijana) 336, Isaya Wlliamu (DB Oratory) 323, Victor Michael (Vijana) 308 na Abdul Kakwaya (DB Oratory) 303.