MWIMBAJI WA KUNDI LA ZABRON SINGERS ‘MARCO’ AFARIKI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Msanii wa Kundi la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Agosti 22, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Jijini Dar es salaam alipokuwa akifanyiwa Upasuaji wa Moyo.

 

 

 

Mwenyekiti wa kundi hilo, Obeid Kazimili amethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa taarifa zaidi itatolewa baada ya taratibu kukamilika.

 

 

“Ninasikitika kutangaza kifo cha mwimbaji mwenzetu ndugu Marco Joseph Bukulu ambaye alikuwa makamu mwenyekiti na Mwalimu Msaidizi wa Zabron Singers kilichotokea usiku wa leo jijini Daresalaam katika hospital ya Jakaya.

 

 

 

“Taarifa zaidi tutazitoa hapo baadae za taratibu za maziko . Bwana awabariki” alisema taarifa ya Obeid Kazimili.

 

 

 

Kundi hilo ni maarufu kwa utunzi wa nyimbo nyingi nzuri kama “Tumeuona Mkono wako Bwana” na “Sweetie Sweetie”.

Related Posts