JESCA Lenga wa timu ya DB Troncatti anaongoza upande wa wanawake kwa kutoa ‘asisti’ nyingi akifanya hivyo mara 193, katika ligi ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
Utoaji wa ‘asisti’ ni pale mchezaji anapotoa pasi kwa mchezaji mwenzake na kisha mwenzake huyo akafunga pointi.
Anayemfuatia ni Tukusubila Mwalusamba kutoka Tausi Royals aliyetoa asisti mara 123, Noela Renatus (Vijana Queens) 98, Tumwagile Joshua (DB Troncatti) 87.
Wachezaji wengine ni Rehema Silomba (DB Lioness) 74, Tumaini Ndossi ( Vijana Queens) 73, Maria Boniventure (Pazi Queens) 73, Nasra Bakari (DB Troncatti) 72 na Juliana Sambwe (Tausi Royals) 71.
Kwa upande wa ufungaji katika maeneo ya mitupo ya pointi tatu (three pointers), anayeongoza ni Diana Mwendi aliyefunga mara 73.
Three point ni maeneo ambayo mchezaji anafunga akiwa nje ya “D” ama nusu duara ya goli.
Anayemfuatia ni Khadija Kalambo (Vijana Queens) aliyefunga three pointer 52, Jesca Ngisaise (JKT Stars) 39 na Irene Gerwin (DB Troncatti) 34. Wengine ni Maria Boniventure (Pazi Queens) 33, Elihaki Joseph (DB Troncatti) 27 na Zena Ahmed (Ukonga Queens) 26.