Klabu ya Wydad Athletic ya nchini Morocco imeendelea kukomaa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Clement Mzize wa klabu ya Yanga ikiwa katika kujenga kikosi chake ili kurejesha ufalme wake uliopotea barani Afrika.
Wydad imewasiliana na Yanga ikiwapa ofa ya dola laki moja ambazo ni takribani milioni 271 ambazo Yanga imezikataa ikihitaji shilingi billion 2.7 ili kukamilisha usajili huo.
Kutokana na klabu hiyo kumhitaji mchezaji huyo kwa udi na uvumba sasa imekuja na ofa nyingine ya dola laki mbili ambazo zinakadiriwa kufikia milioni 5 na ushee huku kukiwa na vipengele vya kuongezea hela hiyo mpaka kufikia billioni 1.3 Kutokana na kiwango cha mchezaji huyo.
Kambi ya Yanga sc ikiongozwa na Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said imetoa msimamo wake kuwa mchezaji huyo hauzwi zaidi ya klabu inayomhitaji kulipa bilioni 2.7 zilizopo katika mkataba wake ili kumpata.
Wawaklishi wa Mzize bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa dili hili linafanikiwa baada ya mchezaji huyo kuonyesha nia ya kukubaliana na dili la kwenda Wydad Athletic inayonolewa na kocha Rulani Mokwena.