KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA MAJI KWA UBUNIFU WA HATIFUNGANI YA TANGA UWASA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Kamati ya Kudumu ya Bunge Maji na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jackson Kiswaga Mbunge wa Jimbo la Kalenga

katika kikao chake imetoa pongezi kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) , pamoja na menejimenti ya Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) kwa kufanikisha ubunifu na uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya TANGA UWASA.

Akitoa taarifa ya katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa TANGA UWASA, Mhandisi Geofrey Hilly amefafanua kuwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TANGA UWASA) katika kuendelea kuboresha huduma zake kwa jamii imeendelea kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo utekelezaji wa mradi wa kuboresha miundombinu ya maji Tanga kupitia uuzaji wa Hatifungani, ambao umetoa fursa kwa jamii kushiriki katika uwekezaji kupitia ununuzi wa hisa hivyo kufanikisha upatikanaji wa fedha zitakazotumika katika utekelezaji wa mradi wa miradi ya maji

Mradi utakaotekelezwa unathamani ya Shilingi Bilioni 53.12 na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mapema mwaka 2024 ambapo unalenga ;

Kuboresha miundombinu katika kituo cha kuzalisha na kusambaza Maji cha Mowe, kuboresha Miundombinu ya mabomba ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga, Mji wa Muheza, Pangani na Mkinga, Kufunga Mita za Malipo ya kabla (Smart Prepaid Water meters) kwa wateja 10,000 na , kuendeleza jitihada za utunzaji wa vyanzo vya maji..

Mapema Februari, 2024 Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango alizindua rasmi Dirisha la uuzaji wa Hatifungani ya Kijani ya TANGA UWASA, ambapo makusanyo ya mauzo hayo yalizidi lengo kwa asilimia 103 ambapo TANGA UWASA ilifanikiwa kukusanya Shilingi za Bilioni 54.72 ambapo lengo halisia lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 53.12.

#KonceptTvUpdates

Related Posts