Mapya kesi ya maujia ya mtoto Asimwe,watuhumiwa wadai hawajui kosa lao mpaka kukamatwa

Ni muendelezo wa ripoti ya kesi ya washitakiwa tisa wa mauaji ya mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu may 30,2024 na June 17,2024 mwili wake ulikutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake

Washitakiwa hao tisa leo August 23 wamefikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwa ajili ya kutajwa tena shtaka lao

Wakili wa serikali Erick Mabagala amesema kuwa mnamo August 21 mwaka huu 2024 walipeleka maombi Mahakama Kuu yenye namba 23143 ya mwaka 2024 wakiomba shauri hilo kuanza kusikilizwa ikiwa ni pamoja na kuomba taarifa za mashahidi zisitolewe katika umma,na kuongeza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba iliridhia maombi hayo mbele ya Jaji Malata.

Aidha Wakili Mabagala amesema kuwa Jaji alitoa maelekezo ya kuzingatiwa baada ya maombi hayo ambayo ni pamoja na kufichwa kwa majina na anuanwi za mashahidi watakapoanza kusikilizwa,taarifa za anuanwi na makazi hazitachapishwa kwa umma,baadhi ya mashahidi watasikilizwa kwa kificho na sura zao hazitaonekana wala kutajwa majina yao.

Baada ya maelekezo hayo upande wa Jamhuri wameomba kupewa muda wa kubadilisha hati ya mashtaka ili iendane na taratibu za mahakama Kuu hivyo wakaomba kutajiwa tarehe nyingine.

Washitakiwa hao wameiomba Mahakama mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona kutajiwa kosa lao huku wakidai hawajui kwa nini wanashitakiwa sambamba na kuiomba Jamhuri kuongeza nguvu katika kukamilisha mwenendo kabidhi ili waweze kujua hatima yao

Wakili wa Serikali Erick Mabagala amewakumbusha shitaka lao kuwa wanakabiliwa na kosa la mauaji ambapo tarahe 30/5/2024 katika eneo la Bulamula kata ya Kamachumu inadaiwa walimuua mtoto Asimwe Novart kwa kukusudia.

Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri,Novat Venant miaka 24 ambaye ni baba wa mtoto Asimwe,Nurdin Ahmada,Ramadhan Selestine,Rwenyagira Alphonce,Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist

Watuhumiwa hao tisa wamerudishwa rumande mpaka september 6 ambapo kesi yao itaitwa tena.

Related Posts