RAIS DKT. SAMIA AKABIDHI CHETI CHA USHIRIKI WA TAMASHA LA KIZIMKAZI 2024 KWA NSSF

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, cheti cha ushiriki wa Tamasha la Kizimkazi 2024. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma wa NSSF, Bi. Lulu Mengele.

Kupitia Tamasha hilo, NSSF imeunga mkono ajenda ya kilimo biashara kwa ajili ya kuwainua wakulima ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja ambao utawapa kipato na kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo ikiwemo kuweka akiba katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ukiwemo NSSF na kukuza utalii wa ndani.


Related Posts