RC Chalamila apiga kambi ya masaa mawili kwa Shoe Shine

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza katika sehemu ya Shoe Shine alipofika Kwa ajili ya kungarisha Viatu na kupata maoni ya wananchi.

*Asema anajifunza vitu vingine na kupata mawazo ya namna ya kuijenga Dar

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefanya kitu kipya katika Mkoa wa Dar es Salaam kutembelea sehemu ya Shoe Shine maarufu kwa Mussa katikati ya jiji Dar es Salaam kuweza kupata maoni ya wananchi.
Akizungumza katika wananchi waliofika kuhakikisha uwepo Mkuu wa Mkoa Chalamila amesema kuwa kukaa ofisini kuna vitu vingine hawezi kuvijua lakini kuonana watu tofauti anapata mawazo ya nini Dar es Salaam inatakiwa kuwa viwango vya juu katika masuala ya utendaji.
Chalamila amesema kuwa katika kufika hapo amejifunza vitu vingi ambavyo ni changamoto za kwenda kushughulikia.
Aidha amesema kuwa Mkuu wa Mkoa sio Simba wa kuogopwa hivyo watu wakimuona wajue yupo ajili ya kusikiliza wananchi.
Hata hivyo amesema kuwa kuna watu wanaweza kuwa na shida ya Mkuu wa Mkoa wasiweze kumuona hivyo kuzunguka na kukutana na watu hao ni rahisi kutoa changamoto zao.
Hata hivyo amesema kuwa suala la uchumi lazima liangaliwe vizuri na sio kubishana katika siasa na Mpira ni jambo ambalo ni starehe baada ya mtu kufanya uzalishaji ambapo linakuwa na kipindi kifupi na sio wakati wote ni siasa.
Mkuu wa Mkoa huyo alitaka wananchi na makundi mbalimbali kuona Serikali iko Kwa ajili yao na wanapoona changamoto kuzipeleka katika kufanya utatuzi ambao utasaidia kupata maendeleo.
Mkuu wa Mkoa amesema katika mazingira ya kawaida mgambo wanakula rushwa kwa machinga kutokana na kuwakamata na kuanza kufanya majadiliano ya kuwalipa.

Related Posts