Simba, Fountain kama kawa Bara

KAMA ulikuwa una presha ya kwenda kwenye Uwanja wa KMC Complex, kucheki gemu ya Simba na Fountain Gate baada ya awali kuwepo kwa hatihati ya kupigwa, we jipange tu, kwani mchezo huo utapigwa kama kawaida keshokutwa Jumapili.

Awali kulikuwa na presha kwamba huenda mchezo huo usingechezwa kama iklivyotokea ule wa Namungo dhidi ya Fountain Gate iliyokuwa na tatizo la usajili wa nyota wa timu hiyo kutokana na kupigwa stop na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), lakini adhabu hiyo imeshafutwa na goma litapigwa kama kawaida.

Taarifa ambazo Mwanaspoti lilipenyezewa mapema leo asubuhi ni kwamba, Faountain Gate imefutiwa adhabu baada ya kumalizana na aliyekuwa nyota kutoka Mbrazili, Rodrigo Figueiredo Calvalho aliyekuwa ameshalipwa lakini hakuwawasilisha taarifa Fifa ili kuiacha huru klabu hiyo iliyokuwa ikifahamika kama Singida Faountain Gate.

Kwa mujibu wa taarifa hizo inaelezwa kwa sasa wameondolewa kizuizi hicho kutokana na kumalizana na kesi hiyo hivyo wamewashiwa taa ya kijani na Fifa kupitia Shirikisho la soka nchini (TFF) huku muda wowote ikitarajiwa kutolewa taarifa rasmi kama ilivyokuwa awali.

Mara baada ya kuwashiwa taa hiyo ya kijani, Fountain Gate imeripotiwa imestua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabiliana na Mnyama aliyeanza kwa kishindo msimu mpya kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United, mchezo uliopigwa hapo hapo KMC.

Walipotafutwa viongozi wa Fountain, walithibitisha kuwa jijini hapa (Dar) lakini hawakutaka kueleza juu ya kuondolewa kizuizi cha kucheza michezo yake ya ligi wakiadai wenye jukumu la kusema hilo ni TFF, japo walikubali kupokea maelekezo ya kuwepo kwa mchezo wao dhidi ya Simba.

“Tulishaambiwa kwamba mchezo utakuwepo hivyo tuendelee na taratibu zetu za maandalizi kama timu  kwa sababu kila kitu kipo freshi, kilichobakia ni TFF tu kutangaza rasmi,” alisema miongoni mwa viongozi wa timu hiyo.

Awali juzi, viongozi wa klabu hiyo walikaririwa walikuwa wakihaha kuona wanalithibitishia Fifa kwamba wameshamalizana na Mbrazili ili mechi hiyo ya raundi ya pili ipigwe, huku Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo alisema walikuwa wanaisikilizia TFF kwani wanataka ratiba iende kama ilivyopangwa baada ya changamoto ya kushindwa kupigwa kwa Namungo na Fountain wikiendi iliyopita.

Related Posts