Tanzania Prisons, Mashujaa hakuna mbabe

Maafande wa Tanzania Prisons wameambulia pointi nyingine ya ugenini, wakilazimisha suluhu dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa raundi ya pili wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma.

Hii mechi ya pili kwa Prisons kutoka suluhu baada ya awali kuibana Pamba Jiji, uliopigwa jijini Mwanza katika ufunguzi wa Ligi hiyo, wikiendi iliyopita, hivyo kuifanya iondoke ugenini ikivuna pointi mbili.

Mashujaa kwa matokeo hayo imefikisha pointi nne, baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 mbele ya Dodoma Jiji katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika, juma lililopita.

Kwa mantiki hiyo, Mashujaa imerudi tena kileleni baada ya awali kutolewa na Singida Black Stars iliyoichapa KenGold, kabla ya yenyewe kutolewa na Simba iliyoanza na ushindi dhidi ya Tabora United ambazo kesho Jumamosi na Jumapili zitakuwa tena viwanjani.

Related Posts