WASHIRIKI wasiopungua 1200 wanatarajiwa kushiriki mbio za barabarani zitakazofanyika Agosti 31 mwaka huu zitakazoanza kutimua vumbi Police Office Mess Masaki.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa The Runners Club, Godfery Mwangungulu ambao ndio waandaaji wa mbio hizo
Alisema ni msimu wa saba sasa wa mbio hizo lakini kwa msimu huu zimekuwa na utofauti.
Mwangungulu alisema mbio hizo za kipekee zitafanyika kuanzia saa 4 kamili usiku hadi saa 6 zikihusisha kilomita 10 hadi 15.
Aliongeza kuwa utofauti wa mbio hizo na zile zingine ni kuwa The Runners zipo kiburudani zaidi kwani baada ya mbio washiriki watakaa na kujipongeza.
“Mbio hizi zina maudhui tofauti, muda wowote unaweza kufanya mazoezi na limekaa kiburudani zaidi na kwa yeyote ambaye atahitaji kushiriki basi atajiunga kupitia kurasa zetu na kuna jezi tumezizindua ambazo zitahusika kwenye mbio hizo.”