CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kimeendelea kupasuka katika Jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya wanachama wao 105 kutimkia ccm.
Wakipokelewa wanachama hao na Katibu wa CCM mkoa, Mercy Mollel katika mkutano wa hadhara kata ya Mwika kusini alisema kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi itaendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na daftari la mkazi ili kupata sita ya kushiriki kuchagua viongozi wa serikali za mitaa badae mwaka huu pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.
Katibu huyo aliwataka wananchi kuepuka kurubuniwa na watu wachache ambao wameanza kujipitisha kutangaza kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani kwani kwa sasa viongozi hao wapo na watekeleza majukumu yao kwa kiwango kikubwa.
“Wanaccm ni lazima tujiandae kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwasimamisha watu wazuri na waadilifu wanaokubalika na makundi yote na sio kusimamisha watu kwa kuangalia Dini, kabila, au undugu” Alisema Mollel.