RC KIHONGOSI ATAKA WANANCHI KUWA MABALOZI WA AMANI ,WAEPUKE VURUGU

Na Mwandishi Wetu,Simiyu

WANANCHI wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kuwa mabalozi wa amani katika maeneo yao sambamba na kuendelea kudumisha umoja, amanI na mshikamano.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi alipokuwa akizungumza na na baadhi ya wananchi wa Lamadi mkoani hapo baada ya kukutana nao katika eneo lililokuwa vurugu.

Kihongosi amesema ni vema wananchi wakawa mstari wa mbele kulinda amani badala ya kuwa vyanzo vya kusababisha uvunjifu wa amani.

“Kuna baadhi ya wananchi wamekiwa wakisababisha vurugu na kukwamisha shughuli za kimaendeleo.Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Simiyu tuwe mabalozi wa amani,tusiwe chanzo Cha uvunjifu wa amani yetu,”amesema Kihongosi.

Akifafanua zaidi Kihongosi amewataka kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa za wahalifu ,wapiga ramli chonganishi pamoja na watu wanaochochea vurugu ili amani iendelee kutawala.

Wakati akitoa kauli hiyo baadhi ya wananchi walikuwa wakifanya vurugu katika Ofisi za Uhamiaji kama sehemu ya kufikisha malalamiko ya kupotea kwa watu lakini amefanikiwa kudhibiti vurugu.” Niwatake wananchi tushirikiane kulinda amani yetu,vyombo vya ulinzi vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha Taifa linakuwa salama.”

Ameongeza amesema hakuna sababu ya wananchi kubeba silaha kupambana na vyombo vya ulinzi na kufanua wakati wananchi wamelala vyombo hivyo vya ulinzi muda wote viko macho kulinda usalama.Pia amesema waleta fujo katika maeneo mbalimbali ni vema wakatajwa badala ya kuwaacha wawe chanzo cha kuvuruga utulivu uliopo.

Related Posts