VODACOM TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA HUAWEI YAZINDUA PROGRAM YA DIGITRUCK KULETA UFANISI ZAIDI UCHUMI WA KIDIJITALI TANZANIA

DigiTruck, darasa la kidijitali linalotembea, litazinduliwa nchini Tanzania mnamo Agosti 2024 kama sehemu ya mpango wa Vodacom Twende Butiama Cycling Tour 2024. Mradi huu ni matokeo ya ushirikiano kati ya Huawei na Vodacom Tanzania, ukiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania kwa ujuzi wa msingi wa kidijitali na kuboresha maarifa yao. DigiTruck inalenga kuwafikia wanafunzi zaidi ya 5,500, wanawake, na vijana katika mikoa 10 nchini kila mwaka, kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Programu ya DigiTruck itatoa uzoefu wa kujifunza unaolenga kubadilisha maisha kupitia vipindi viwili maalum:

1. Programu ya Siku 6: Hii inalenga wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri wa miaka 16 hadi 19.

2. Programu ya Wiki 2: Inalenga vijana waliojiajiri na wanawake wajasiriamali wenye umri wa miaka 20 na zaidi.

DigiTruck ni hatua kubwa ya kubadilisha upatikanaji wa elimu ya kidijitali nchini Tanzania, hasa kwa maeneo yenye upungufu wa fursa. Mradi huu unalenga kuleta usawa katika elimu kwa kuhakikisha kuwa vijana na wanawake wanapata ujuzi muhimu wa kidijitali ambao utawasaidia kufanikiwa katika ulimwengu wa sasa unaoendelea kubadilika kidijitali.

Baada ya mafanikio makubwa ya DigiTruck nchini Ethiopia, Ghana, Uganda, na Kenya katika miaka mitatu na nusu iliyopita, sasa ni wakati wa Tanzania kufaidika na mpango huu wa kibunifu. DigiTruck inaonesha dhamira ya Huawei na Vodacom ya kuwawezesha Watanzania wote, bila kujali mahali wanapotoka, kupata ujuzi muhimu wa kidijitali na kujiandaa vyema kwa maisha ya kidijitali yanayokuja.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts