NCBA golf series imerudi tena kwa kishindo

Kwa mara nyingine tena michuano ya mchezo wa Golf Tanzania maaarufu kama NCBA Golf imerejea kwa kishindo, ambapo ikiwa ni wiki chache baada ya awamu ya kwanza ya mashindano hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro kurindima huko jijini Arusha tarehe 29 Julai.

 

Mashindano ya NCBA Golf Series jijini Dar es Salaam yanatarajiwa kuleta ushindani wa kusisimua zaidi kwa kukusanya pamoja vipaji mbalimbali vya gofu kutoka pande mbalimbali za Dar Es Salaam. Mashindano ya mwaka huu ambayo  yatahudhuriwa na viongozi wa kampuni mbalimbali, mashirika yasiyo ya serikali na wadau, mshindi atazawadiwa kiasi cha pesa taslimu pamoja na begi la gofu lenye thamani ya Shilingi milioni 3 za Kitanzania.Aidha, kwa gharama za waandaaji mshindi atapata nafasi ya kwenda Nairobi kuhudhuria Fainali Kuu ya NCBA Golf Series mwezi Novemba.

Akizungumza kuhusu mashindano hayo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro, Ameeleza kuwa mashindano hayo yanasaidia kukutanisha wachezaji mbalimbali wa Golf na kusaidia kuvumbua vipaji vipya vya wachezaji wa Golf huku akisifia juhudi za waandaqaji wa mashindano hayo kwa kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa

Related Posts