Rais Samia ataka CHAN ipigwe Samia Suluhu Sports

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Uwanja wa Samia Suluhu Sports Academy kukamilika Januari 2025 badala ya Aprili ili uweze kutumika katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) inapigwa katika uwanja huo.

“Tarehe 22, niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Suluhu Sports Academy unaotarajiwa kukamilika kwa ratiba Aprili 2025, lakini nimemhimiza Mwenyekiti anayesimamia ndugu Abdul Majid Nsekela uwanja huu ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 20,000, aukamilishe ifikapo Januari, mwakani ili Februari CHAN iweze kuchezwa ndani ya Kizimkazi jimbo la Makunduchi.

“Mradi huu utakuwa na michezo ya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, netiball, kuogelea, riadha na mengine kwa viwango vya kimataifa na umedhaminiwa na wadau wa maendeleo ndani ya nchi wakiongozwa na CRDB Foundation,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumapili Agosti 25,2024 wakati akifunga kilele cha Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Unguja visiwani Zanzibar likiwa na Kaulimbiu ya Kizimkazi Imeitika.

Related Posts