Wanafunzi sita wa Shule ya Msingi Ochuna Wilaya ya Rorya mkoani Mara wamefariki dunia wakidaiwa kuzama na kunasa kwenye tope katika bwawa la skimu ya kilimo cha umwagiliaji lililopo kijijini hapo.
Watoto hao wakiwemo watatu wa familia moja wote ni wakazi wa kijiji cha Ochuna.
Tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 24, 2024 jioni baada ya watoto hao kufika kwenye bwawa hilo kwa ajili ya kuogelea
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema wakiwa wanaogelea bwawani humo watoto hao walijikuta wakisogea hadi kwenye kina kirefu kisha kunasa kwenye tope.
“Walikuwa watoto saba mmoja aliondoka kabla ya tukio na wengine waliendelea na kisha kunasa kabla ya kufariki dunia,” amesema DC Chikoka.
Amefafanua kuwa miili yote imeopolewa na taratibu za mazishi zinafanyika kijijini hapo kwa uratibu wa serikali ya wilaya.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.