Wanane wafariki dunia, zaidi ya 12 wajeruhiwa ajali ya Hiace Mara

Watu wanane wamefariki dunia huku wengine zaidi ya 12 wakijeruhiwa katika ajali iliyotekea Kijiji cha Kyandege wilayani Bunda Mkoa wa Mara.

Ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Toyota Hiace iliyokuwa  ikitokea mjini Mugumu wilayani Serengeti kwenda wilayani Bunda, imetokea leo Jumapili Agosti 25, 2024 saa 11.30 jioni.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema katika ajali hiyo watu wanane wamefariki, wakiwamo saba  waliofariki papo hapo  na mmoja kufariki akiwa anapatiwa matibabu hospitalini.

Dk Naano amefafanua kuwa miongoni mwa waliofariki ni wanawake watano huku wanaume wakiwa ni watatu.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliosababisha tairi la nyuma kupasuka na kisha gari kukosa mwelekeo.

“Gari limepinduka mara kadhaa na liliposisimama likageuka kuangalia kule lilipokuwa linatokea,” amesema Dk Naano.

Amesema majeruhi wamelazwa katika vituo tofauti vya kutolea huduma za afya katika wilaya za Bunda na Serengeti.

Related Posts