DC TEMEKE AWAFYATUKIA WATENDAJI WA MITAA “MNAWEZA MSIIONE PEPO” – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mkuu wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda ametoa maelekezo kwa mabalozi wa mitaa kutojihusisha na shughuli za uuzaji viwanja kwa Sababu zimekuwa ni kichocheo cha migogoro kwenye maeneo yao.

DC Mapunda ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi wa Toangoma, kupitia mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza na Kutatua Kero zao mbalimbali.

“Haiwezekani manispaa ikaona eneo ni hatarishi yaani kwa matumizi ya Serikali ni hatarishi kwa mtu binafsi si hatarishi, kesho ikimkuta hatari serikali itamlipa gharama kwa sababu maji yamejaa tulimwambia alipie kodi na hati tumempa tunaiingiza Serikali matatizoni tusifike huko” amekemea DC Mapunda.

Sambamba na hilo, DC Mapunda ametoa tahadhari kwa wakazi wanaojenga kwenye maeneo hatarishi hasa katika bonge la vikunai, ambapo amesema kuwepo kwa ujenzi wa nyumba za makazi katika eneo hilo sio salama.

Related Posts