Mtoto Mchanga ameokolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dodoma baada ya mama yake aitwae Catherine Iwaho kumtupa mtoto huyo chooni. Mara baada ya mtoto huyo kuokolewa alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) kwa Matibabu zaidi Agosti 26, 2024
Tukio Hilo limetokea maeneo ya Ipagala ambapo mtoto huyo amekutwa akiwa hai. Akitoa taarifa ya tukio hilo Mkaguzi Deogratius Inano amesema Baada ya kuvunja sehemu ya choo hicho majira ya Asubuhi walikumkuta mtoto huyo.
Aidha, Naibu Kamishna Puyo Nzalayaimisi akiambatana na Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma Mrakibu Rehema Menda wamemtembelea na Kumjulia hali Mtoto huyo ambaye anaendelea na Matibabu katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa
“Sisi Jeshi la Zimamoto tunakemea na kulaani Vikali kabisa juu ya suala hili la kutupa watoto chooni au kwenye mashimo ya taka, kila mtu anahaki ya kuishi kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza” amesema DCF Nzalayaimisi