Katika jitihada zakutoa elimu kwa wananchi kufahamu haki ya kuhoji juu ya mienendo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao , taasisi ya Wajibu imezindua mradi wa NINAWAJIBIKA unaolenga kutoa hamasa kwa wananchi kujikita katika kuhakikisha wanajenga utaratibu wakuwajibika kikamilifu kufahamu mapato na matumizi ya miradi mbalimbali katika jamii kwani wanahaki yakujua gharama zote ikiwa maendeleo yote hutokana na kodi mbalimbali wanazozitoa.
Akizindua mradi huo kwa niaba ya katibu tawala wa Wilaya ya Mbinga, Afisa Tarafa ya Kigonsera Mh. Focus Jacob amezungumzia umuhimu wa kutambua na kushiriki katika utambuzi wa miradi yote inayotekelezwa kwenye maeneo yao jambo ambalo husaidia kuepusha migogoro mbalimbali ambayo hujitokeza katika jamiii kwakushindwa kuwashirikisha wananchi katika miradi mbalimbali.
Ameeleza kuwa jukumu lakulinda miradi nilawananchi kwa ujumla kwa kuhakikisha kila mwananchi anakuwa mlinzi katika jitihada zakufanikisha miradi hiyo inaendelea kulindwa huku akiwataka viongozi kufahamu nafasi walizonazo zinatokana na uwepo wa wananchi hivyo washirikiane kwaumoja wao ili kufanikisha utekelezaji wa mradi wa NINAWAJIBIKA.
Awali Akitoa elimu kwa baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali kutoka kigonsera, Mkako na Lipumba, Mkurugenzi wa mtandao wa utawala bora Dkt Denis Mpagaze, amesema kuwa wananchi wanatakiwa kufahamu haki zao kikatiba pamoja na kuwawajibisha viongozi wasio waadilifu kwakuzingatia matumizi sahihi ya lugha nzuri na zenye maadili, kwani wanapaswa kuwa na uchungu na kodi wanazolipa kwakuhakikisha zinatumika katika matumizi sahihi.
Kufuatia elimu hiyo wananchi wamefurahishwa na uzinduzi wa mradi huo ambao utawajengea ujasiri wakuhoji mapato na matumizi nakuahidi watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wengine kwakuhakikisha elimu waliyoipata wanaifikisha kwa jamii jambo ambalo litachochea uwajibikaji.
Imeelezwa kuwa mradi wa NINAWAJIBIKA utatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili kwenye maeneo yote ya Kigonsera, Mkako na Lipumba ambapo watahakikisha elimu inawafikia kikamilifu wananchi pamoja nakuwajengea utaratibu wakuwajibika kwakuhoji kila kitu kinachofanyika kwenye maeneo yao.