JKT Stars yaitembezea kichapo Vijana Queens

TIMU ya JKT Stars imeifunga Vijana Queens kwa pointi 73-56 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam uliochezwa kwenye Uwanja wa Donbosco Osterbay na kuacha maswali kwa wapenzi wakiijadili timu hiyo kongwe.

Hata hivyo mchezo huo ulitaka uingie dosari kutofanyika  kutokana na wachezaji wa Vijana Queens kuamini hivyo.

Picha hiyo ilionekana pale baadhi ya wachezaji waliowahi kufika uwanjani kuonekana hawapo kiushindani, jambo ambalo siyo la kawaida, kwani kila timu inapofika huonyesha amshaamsha.

Baadaye wachezaji walimweleza kamishina wa Ufundi wa Mashindano hayo, Haleluya Kavalambi kuwa wameelezwa na viongozi wao kwamba mchezo hautakuwepo.

Baadaye Kavalambi aliwaonyesha ratiba ya mashindano iliyotumwa kwa viongozi wa klabu, ikionyesha kuwepo kwa mchezo huo.

Baada ya kuambiwa na Kavalambi hivyo, wachezaji waliofika mapema Boke na Tumaini Ndosi walianza kazi ya kuwapigia simu wachezaji wengine.

Wakati Vijana Queens wakijikusanya, JKT Stars ilifika uwanjani saa moja kabla ya mchezo kuanza na kuanza kupasha.

Katika mchezo huo Vijana Queens ilianza mchezo katika robo ya kwanza kwa kuonyesha haikuwa imejiandaa na mchezo hali iliyoifanya JKT Stars itumie upungufu huo kuongoza kwa pointi 24-14.

Robo ya pili Vijana Queens ilijitutumua na kufanikiwa kupata pointi 16-9 ilhali ile ya tatu JKT Stars ilipata pointi 18-11 na 22-15.

Katika mchezo huo, Wande Ibrahim wa JKT Stars alifunga pointi 18 akifuatiwa na Jesca Ngisaise aliyefunga pointi 15.

Kwa upande wa Vijana Queens alikuwa ni Noela Renatus aliyefunga pointi 20 akifuatiwa na Ndossi aliyefunga 14.

Mchezo mwingine uliochezwa uwanjani hapo ulishuhudia Tausi Royals ikiifunga UDSM Queens kwa pointi 63-28.

Related Posts