LATRA watoa tuzo kwa wasafirishaji bora na salama wa mabasi

Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mhe. Daniel Baran Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Agosti 26, 2024 wamekabidhi tuzo kwa wasafirishaji Bora na Salama kwa mabasi ya njia ndefu katika sherehe za ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Tuzo hizo zimetolewa kufuatia shindano la kutafuta Watoa huduma Bora na Salama kwa huduma zilizotolewa Juni, 2023 hadi Julai 2024 kwa makundi ya Wasafirishaji Wakubwa, Wakati na wadogo lililoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ikiwa ni sehemu ya kuchochea ufanisi katika huduma za usafiri wa mabasi.

Related Posts