Mabeki wageuka tishio kutupia nyavuni BDL

WAKATI timu zote zikiwa zimecheza michezo 26 ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kuna vita mpya imeonekana kuwapo kwa wachezaji wanne wanaocheza nafasi ya ulinzi namba 4 maarufu kama center wanaoonekana kuwa tishio katika wa kufunga.

Wachezaji hao ni Haji Mbengu wa Dar City, Jimmy Brown (UDSM Outsiders), Fotius Ngaiza (Vijana) na Jordan Jordan  anayeichezea Mchenga Star.

Wachezaji hao wanacheza nafasi ya ulinzi sifa yao kubwa nyingine imekuwa kudaka mipira yote inayofika golini kwao (rebounder), kuzuia mipira (blocks) kwa wapinzani wao wasifunge pamoja na kwenda kufunga.

Rebounder inazungumzwa ni pale mchezaji anapodaka mpira  unaongonga goli na kabla haujashuka chini mchezaji anadaka ilhali block ni pale mchezaji anapozuia mpira kwa mpinzani asiweze kufunga.

Wachezaji waliozoeleka kufunga ni wale wanaocheza nafasi ya kati wakifahamika kimchezo kama point guard pamoja na  wale wa mbele wanaoitwa shooter.

Akizungumzia uwezo huo, Ngaiza ameliambia Mwanasposti kwamba mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi kama yao  anapaswa kuwa na nguvu na kutumia akili ili aweze kufikia malengo.

Related Posts