Kufeli klabu nne CAF tatizo uwekezaji

MDAU wa michezo Masanja Ngwau, ameeleza tatizo kubwa lililozikumba timu nne zilizotolewa mapema kwenye mashindano ya Afrika kwa klabu ni uwezekezaji duni.

Masanja amesema klabu za Zanzibar na hata ile moja nje ya Azam, zimekumbana na kutolewa raundi ya awali kutokana na kukosa maandalizi mazuri ya mashindano hayo na kujikuta zinatolewa mapema.

Mdau huyo ameyabainisha hayo leo Agosti 28, 2024 wakati akichangia mjadala katika Mwananchi Space, inayoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) wenye mada isemayo; ‘Tumekosea wapi timu nne za Tanzania kutolewa mashindano ya klabu Afrika?’

Masanja amesema wadau wa michezo hususani kampuni mbalimbali zinatakiwa kujitokeza kuzisaidia klabu nyingine ambazo zina uchumi wa kati.

Hata hivyo, Masanja hakumalizia vizuri mchango wake baada ya mawasiliano yake kukatika akiwa hewani.

Related Posts