MAKALLA ATAJA SABABU ZA USHINDI WA CCM UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Katibu wa NEC, itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla amewataka Watanzania kuchagua Wagombea wanaotokana na Chama hicho Kwenye Uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa Uliopangwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu nchi nzima.

CPA Makala ametoa Kauli hiyo Agosti 27, 2024 akiwa kwenye ziara yake Wilayani Kigamboni wakati alipokuwa akizungumza na Wananchi kupitia Mkutano wa hadhara.

Amesema zipo sababu za msingi kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi wa heshima na kishindo katika uchaguzi huo wa Serikali Mitaa kwa Sababu ya mafanikio ambayo yamepatikana kwa Wananchi kupitia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020/2025.

“Lengo la Chama cha siasa ambacho kimesajiliwa ni kushika dola, Chama cha siasa ambacho kimesajiliwa hakifanyi kazi ya kuhubiri kuhusu kufika mbinguni maana hiyo ni kazi ya viongozi wa dini huko misikitini na kanisani lakini kazi ya Chama cha siasa ni kukamata dola, Ili ushike dola unatakiwa kushinda chaguzi mbili chaguzi ya Serikali ya Mtaa na uchaguzi Mkuu” amesema CPA. Makalla.

Related Posts